TIGO YADHAMINI NGORONGORO MARATHON


Jumamosi tarehe 14,2012, kwa mara ya tano Mbio za Ngorongoro zitashuhudia wakimbiaji wa kms 21 wakitokaka katika geti la Ngorongoro Crater kupitia milima na mabonde hadi kwenye utepe wa kukamilisha hizi mbio mjini Karatu kwenye ‘ Mbio dhidi ya Malaria.’
“Moja ya vipaumbele vyetu katika programu zetu za kuisaidia jamii Afrika ni kwenye Afya na hali njema” alisema bi Ester Palsgraaf,ambaye ni Meneja Mahusiano na jamii …………………….. “Katika program ya mwaka 2012 tunashirikiana na Zara Charity ili kuwaelimisha watu kuhusu ugonjwa wa malaria,lengo likiwa ni kusaidia kupunguza maambukizi,” alisema.
Mwaka huu Zara Charity wamechukua uongozi wa mbio za Ngorongoro kutoka kwa Minnesota International Health Volunteers (MIHV). Zara Charity inafanya kazi na kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuhakikisha ushiriki wa wanariadha duniani,mpaka sasa wakimbiaji wenye sifa za kimataifa 200 wameshajiandikisha.
Zara charity pia inashirikiana na wizara ya afya na ustawi wa jami kuelimisha watu kuhusu malaria kabla ya siku ya malaria duniani tarehe 25 mwezi wa nne 2012. Mbio hizi zinaonekana kama nafasi ya kueneza uelewa kuhusu malaria na juhudi za moja kwa moja za kupambana na ugonjwa huu unaozuilika

“Tumefurahishwa sana na ushirikiano ambao tumeupata kutoka mashirika tunayofanya nayo kazi” alisema bwana Silevery Tesha mratibu wa Zara Charity. “Tunajua jinsi gani malaria ilivyo na athari Tanzania na ndiyo maana tumejitoa kuupiga vita. Mbio hizi zitatumia njia ya kufurahisha kuleta uelewa wa tatizo hili na tunafuraha mwaka huu kwa timu ya olimpiki ya Tanzania kushiriki katika mbio hizi kama moja ya maandalizi ya olimpiki za London Julai hii” alisema.

Waandaaji wa mbio hizi wamepanga kuwa na zaidi ya timu za makampuni 50, ikiwa ni pamoja na kuandaa mbio za kawaida kwa watoto wa umri wa wanafunzi wa shule za msingi kushiriki katika mbio za kilometa 2.5. Mbio zote zitaanza saa 2:30 asubuhi
Malaria ni ugonjwa hatari ambao unaua watu milioni moja hadi tatu kwa mwaka na kusababisha vifo 3000 vya watoto kila siku, inaendelea kuwa moja ya magonjwa yanayoongoza kwa kuua duniani. Waathirika wakubwa wakiwa ni watoto chini ya miaka mitano na kina mama wajawazito.

Kuhusu Tigo
Tigo, the first cellular network in Tanzania, started operations in 1994 and is Tanzania’s most affordable and innovative mobile phone operator covering 26 regions in mainland Tanzania and Zanzibar.
Tigo is part of Millicom International Cellular S.A (MIC) which provides affordable, widely accessible and readily available cellular telephony services to more than 43 million customers in 13 emerging markets in Africa and Latin America.
For further information visit: www.tigo.co.tz
Mratibu wa Promosheni na Matukio wa Kampuni ya tigo Eduward Shilla akizungumza kuhusu mashindano ya mbio za Ngiorongoro

Post a Comment

Previous Post Next Post