CHUJI ATOROSHA WENZAKE A-TOWN

WAKATI baadhi ya viongozi wa timu ya Yanga walishikiliwa mkoani Arusha kwa ajili ya deni la hoteli waliyofikia pamoja na wechazi katikati ya wiki hii, kiungo wa timu hiyo Athuman Idd Chuji alitumia umafia kuwatorosha wenzake.
Yanga ambayo ilikuwa mkoani humo kukwaana na JKT Oljoro na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, ilijikuta ikizuiwa kuondoka baada ya kuwepo kwa deni katika hotelki waliyofikia.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kuona hali hiyo, Chuji alitumia ujanja wake na hatimaye wachezaji wa timu hiyo walitoroka na kurejea jijini Dar es Salaam.
"Yaani hali si hali ndani ya klabu byetu ona mpaka inafikia wachezaji na viongozi wanazuiwa kwa deni la hoteli, kama si chuji wachezaji wangeendelea kusota Arusha", alisema mwanachama mmoja.
Yanga ambayo imeweka rehani ubingwa wa ligi kuu bara baada ya kutetereka katika ligi hiyo, kwa sasa inakabiliwqa na ukata wa hali ya juu.
Kama hiyo haitoshi mambno ndani ya klabu hiyo si shwari kiasi cha baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji kujiuzulu, kabla ya baraza la wazee kuichukua timu hiyo kwa lengo la kuinusuru.

Post a Comment

Previous Post Next Post