WAKATI
pambano la kuwania bingwa wa ngumi unaotambuliwa na IBF Africa kati ya Mada
Maugo na Francis Cheka ukitarajiwa kufanyika kesho kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba,
mabondia hao kila mmoja ametamba kumtwanga mwenzake.
Mabondia
hao watapambana katika uzito wa Kati, katika pambano la raundi 12 ambapo pamoja
na ubingwa mshindi ataondoka na gari aina ya Toyota Mark 11 Grande lenye
thamani ya shilingi milioni 8.
Wakizungumza
na mamapipiro blog wakati wa kupima uzito leo, mabondia hao kila mmoja
alitamba kumtwanga mwenzake kwa Ko.
Kwa
upande wake Maugo alisema kuwa kwa maandalizi aliyoyafanya ana uhakika wa
kushinda mpambano huo, lakini akiwaomba waamuzi wafanye haki katika maamuzi yao
ili mshindi apatikane kihalali.
“muda
wa kuongea umekwisha hivyo vimebaki vitendo, nipo tayari kwa mpambano huo
lakini kubwa ni kuwaomba waamuzi kutenda haki na mshindi apatikane
kihalali,”Alisema.
naye
Cheka alisema Maugo si lolote kwake na atamfundisha kazi mapema tu na
amejiandaa ipasavyo na mpambano huo ambao anaamini ataibuka na ushindi.
Naye
mwandaaji wa pambano hilo Lucas Ruta kupitia kampuni ya Kitwe General Traders,
alisema kwamba maandalizi yamekamilika ambapo kutakuwa na ulinzi wa uhakika kwa
mali na mashabiki watakaojitokeza kushuhudia.
Alisema
pambano hilo litatanguliwa na mengine nane ya utangulizi hivyo amewaomba
mashabiki wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi ambapo kundi la Gangwe Mob litatoa
burudani.