Ligi Kuu ya Vodacom inaendelea katika raundi
ya 25 kesho (Aprili 28 mwaka huu) ambapo Coastal Union itakuwa mwenyeji wa
Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga huku Mtibwa Sugar ikiwa
mgeni wa African Lyon kwenye Uwanja wa Chamazi.
Aprili 30 mwaka huu Azam na
Toto African zitacheza Chamazi wakati Mei 1 mwaka huu Villa Squad itaumana na
Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Chamazi.
Ligi hiyo itafunga msimu wa
2011/2012, Mei 5 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa uwanjani. Simba vs Yanga
(Uwanja wa Taifa), Oljoro JKT vs Polisi Dodoma (Sheikh Kaluta Amri Abeid,
Arusha) na Ruvu Shooting vs Villa Squad (Mabatini, Mlandizi).
Mechi nyingine zitakuwa kati
ya Coastal Union vs Toto African (Mkwakwani, Tanga), African Lyon vs JKT Ruvu
(Manungu, Morogoro), Azam vs Kagera Sugar (Chamazi, Dar es Salaam) na Moro
United vs Mtibwa Sugar (Jamhuri, Morogoro).