Wachezaji wawili Watanzania wameombewa Hati
ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu katika nchini
za Denmark na Jamhuri ya Czech.
Chama cha Mpira wa Miguu cha
Denmark (DBU) kimemuombea hati hiyo William Benard Okum kama mchezaji wa ridhaa
ili ajiunge na timu ya Brabrand IF. Klabu ya zamani ya Okum ni Viko Pham FC ya
Zanzibar.
Naye Samwel Jonathan Mbezi
ameombewa hati hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu cha Jamhuri ya Czech (FACR) ili
aweze kuchezea timu ya Sokol Dolany akiwa mchezaji wa ridhaa. Katika maombi
hayo, FACR imeonesha kuwa Mbezi kwa sasa hana timu anayochezea hapa
nchini.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) linafanya mawasiliano na pande husika kabla ya kutoa hati hizo
kwa wachezaji hao kama walivyoomba DBU na FACR.