Promota wa pambano la ngumi baina ya Mada Maugo na Francis Cheka, Lucas Ruta kulia pamoja na pamoja na mmoja ya wadhamini wa pambanmo hilo Yohannes Lugenge kushoto wakionyesha gari pamoja na mkanda atakaovishwa bingwa wa pambano hilo la kuwania mkanda wa IBF Afrika litakalofanyika Aprili 28 kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.
WAKATI zawadi ya gari atakalotwaa bingwa wa ngumi wa mkanda
wa IBF Afrika kati ya Mada Maugo na Francis Cheka likianikwa hadharaji jana, kamisheni
ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) imesema iwapo mshindi wa mpambano huio atabainika kutumia
madawa ya kuongeza nguvu atanyang’anywa zawadi.
Mabondia hao wanatarajia kuzindunda Aprili 28 mwaka huu
katika ukumbi wa PTA Sabasaba katika pambano la raundi 12 uzito wa kati ambalo
limeandaliwa na kampuni ya Kitwe General Traders.
Mratibu wa mpambano
huo Yassin Abdallah ‘Ustadh’ aliiambia mamapipiro blog kwamba mara baada ya mpambvano huo
mabondia wote watapimwa afya zao na iwapo mshindi atabainika kutumia dawa za
kulevya atavuliwa ubingwa.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuleta nidhamu katika
mchezo huo ambao umeonekana kuwa wa kihuni sambamba na kupiga vita utumiaji wa
dawa za kulevya katika michezo.
“Tunapiga vita matumizi ya bangi na dawa zote za kuongeza
nguvu katika michezo hivyo tunaopenda kutoa tahadhari kwa mabondia hawa na
wengineo kuachana na mambo haya kwani watajikuta wakipoteza haki zao za msingi
baada ya kushinda kama watabainika kutumia vitu hivyo,”alisema Ustadhi.
Mratibu huyo aliongeza iwapo mabondia hao watatoa sare,
zawadi hiyo itabaki kwa promota hivyo ni lazima mshindi apatikane katika mpambano huo na amewataka mabondia hao kupigana kwa nguvu
zote.
Aidha, waandaaji wa pambano hilo leo wameonyesha rasmi gari lenye thamani ya shilingi milioni 8 na mkanda ambao atakabidhiwa bingwa wa mpambano huo ambapo kabla ya mabondia
hao kupanda jukwaa kutakuwa na mapambano nane ya utangulizi.
Mgeni rasmi katika mpambano huo anatarajiwa kuwa meya wa
Manispaa ya Ilala Jerry Slaa ambapo kiingilio ni shilingi 10,000 kwa viti
maalum na shilingi 5,000 kwa viti vya kawaida.