Na Rodrick Mushi,Moshi.
Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro limemfukuza kazi askari
wake aliyefanya vurugu disko pamoja na kukutwa na misokoto minne ya bangi.
Akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa
Polisi Mkoani hapa Absalom Mwakyoma
alisema kuwa jeshi hilo limemfukuza rasmi askari huyo baada ya
kufikishwa kwenye mahakama ya kijeshi na kukutwa na makosa mawili ya jinai.
Tukio la askari
aliyefukuzwa kuingua kwenye ukumbi wa starehe na kufanya vurugu lilitokea april
2 mwaka huu baada ya askari huyo ambaye
aliingia eneo hilo majira ya saa 6 usiku na kuanza kufanya vurugu pamoja na
shambulio kwa mmliki wa Christopher Shayo pamoja na mlinzi..
Mwakyoma alisema kuwa askari huyo mwenye namba G8415
Deogratiasi Matious (22) alifanya fujo
na kasha kumshambulia mlizi wa ukumbi wa disko wa Pub Alberto Rajabu Mohamedi na kummuumiza kwa kumngata
kwenye mkono.
Hata hivyo alisema kuwa kosa lingine alilofanya askari huyo
aliyefukuzwa ni pamoja na kukutwa na misokoto 4 ya bangi ikiwa mfukoni
mwake,hivyo makosa hayo mawili ndio yaliyomfukuzisha kazi.
Alisema kuwa jeshi hilo limefanya hivyo kutokana na kuwepo
kwa malalamiko kwa baadhi ya askari kukiuka maadili ya jeshi hilo.
Katika wakati mwingine alisema kuwa baada ya kufukuzwa kazi
atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili,na kazi hiyo imekabidhiwa
kwa mwanasheria wa Serikali ili kulifikisha shauri hilo Mahakamani.
Mwakyoma alisema kuwa kwa mwaka 2011/2012 askari wapatao 18
wameshafukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu ikiwemo kukiuka maaadili ya
Jeshi hilo.