Happiness Katabazi
MSANII wa
Filamu nchini, Kalaja Masanja leo alimwaga machozi na kuuujia juu upande wa
Jamhuri katika kesi inayomkabili ya utakajitishaji fedha haramu katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akiushinikiza ulete mashahidi haraka
kwani kule gerezani anakoishi siyo sehemu ya starehe.
Kajala
alitoa shinikizo hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo muda mfupi baada
ya Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na
Rsuhwa (PCCB), Swai kuikumbukusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwaajili
ya mashahidi wa upande wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao lakini akadai hilo
halitaweza kufanyika kwasababu hajaja na mashahidi na kwamba anaiomba kesi hiyo iarishwe.
Baada ya
wakili huyo wa PCCB kumaliza kutoa maelezo hayo ndipo Kajala akanyosha kidole
na kuomba ruhusa ya mahakama ili aweze kuzungumza jambo na alizungumza kama
ifuatavyo:
“Mweshimiwa
hakimu hivi huyu wakili wa serikali anafikiri kule gereza la Segerea ninakoishi
kwa sasa ni sehemu ya stahere? Gerezani
kunatisha wewe wakili wa serikali lete
mashahidi kesi isikilizwe”alidai Kajala
huku akitokwa na machozi.
Kwa upande
wake Hakimu Fimbo aliarisha kesi hiyo Mei 9 mwaka huu,ambapo upande wa jamhuri
unatakiwa ulete mashahidi wake ili waanze kutoa ushihidi.
Machi 27 mwaka huu, ilidaiwa na wakili Swai kuwa Wakili wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Leonard Swai alidai mbali na Kajala mshtakiwa mwingine ni
muwe Faraja Chambo wanakabiliwa na makosa matatu, kosa la kwanza
ni la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa ya mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo la
kula njama la kuamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala eneo ambalo
halijapimwa jijini Dar es Salaam.
Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki
wa nyumba hiyo ambayo walikuwa wakiimiliki kwenda kwa Emilian Rugalia ambaye
ndiyo walimuuzia kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya TAKUKURU ya
mwaka 2007. Na shtaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda siku
hiyo ya Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo.
Chambo ambaye naye yupo gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kwasababu anakabiliwa
na kesi nyingine ya utakatishaji fedha haramu iliyofunguliwa mahakamani hapo
ambapo kwa mujibu wa sheria kosa hilo halina dhamana.
mwisho