MWIGIZAJI nguli Tanzania, Steven
Kanumba amefariki dunia ghafla nyumbani kwake maeneo ya Sinza Vatican, Dar es
Salaam usiku wa kuamkia leo.
Chanzo kimesema kuwa Kanumba
alifariki wakati akiwa anagombana na mpenzi wake, mwigizaji mwenzake, Lulu.
“Alikuwa anagombana na Lulu. Lulu
akamsukuma Kanumba, akaangukia kichwa, ndio akafa, ilikuwa saa tisa usiku,”kilisema
chanzo.
HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa
Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka
2012.
Elimu ya msingi alipata katika
shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar
Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne
Dar Christian, Kanumba alijiunga na sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia
kwa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee
Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la
Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba
aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe ya filamu na hadi anakutwa na umauti
alikuwa mwigizaji anayefahamika Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa
duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa
wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya
ni Dar To Lagos, She is My Sister, Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu,
Sikitiko Langu, Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na
kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema
atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi
sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika
tasniya ya filamu Tanzania. Taifa limempoteza mtu ambaye alikwishaanza
kuitangaza vema nchi kupitia sanaa hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi
katika anga za kimataifa zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa
filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa
Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa
alifika hadi Hollywood, Marekani, ambayo ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa
mwili wa marehemu upo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Mungu aiweke pema peponi roho ya
marehemu. Amin.
RIP Kanunmba. You will be remembered greatly
ReplyDeleteMimi Ni Mjane, Niliumia mno kifo cha mume wangu, lakini nilikuwa nikimuona Kanumba nafarijika kwani alifanana mno na marehemu mume wangu kama vile ni ndugu. sasa kufariki kwa kanumba nahisi kupata maumivu mara mbili.
ReplyDelete