Kaseja |
NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja, amesema vitimbi
wanavyofanyiwa na wenyeji havitawafanya wapunguze ari ya kushinda pambano lao
dhidi ya Setif kesho.
Akizungumza na tovuti ya Simba, Kaseja alisema wametazama
kwa makini matukio mbalimbali yanayofanywa na wenyeji wao na wamebaini yako
mambo ambayo lengo lake ni kuwaondoa mchezoni.
“Hebu fikiria, watu wanataka kutusafisha kwa basi kwa masaa
sita wakati wanajua kanuni ni masaa mawili tu. Halafu, badala ya kutusafirisha
hadi mji wa Setif tulipocheza, wao wametupeleka kwanza mji mwingine na halafu
wakatusafirisha kwa basi kuja Setif. Hizi ni mbinu zao lakini tunazijua,”
alisema.
Kaseja alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba walioitoa
Zamalek ya Misri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika miaka kumi iliyopita
na anasema hakuna cha ajabu iwapo timu yake itaitoa Setif.
“Katika uzoefu wangu wa soka, timu pekee ya kiarabu ambayo
ilitutendea vema ilikuwa ni Harass Al Hadoud ya Misri miaka miwili iliyopita.
Lakini hawa walikuwa wema kwa sababu walikuwa wametufunga katika mechi ya
kwanza na hivyo hawakuwa na wasiwasi.
“Ukiona Waarabu wanakufanyia vitimbi ujue wana wasiwasi na
wewe. Kama hawana hofu, watakupa kila unachohitaji. Nashukuru kwamba tuna
wachezaji wazoefu wa kutosha wanaoweza kupambana na lolote,” alisema.
KUMBE ZILE HAMSA (5)MLIZOPIGWAGA NA HARRAS AL HADOUD ZILIKU HALALI SASA MBONA HAMKUSEMA KIPINDI KILE MKAJA NA BEGI LA VISINGIZIO KWAMBA MLIHUJUMIWA,KUMBE ILIKUA NI KATIKA JITIHADA ZA KUHALALISHA KIPIGO
ReplyDeleteMDAU WA BOMBA - REVERE,MASACHUSSETTS,USA