Na Mwandishi Wetu
KUNDI la muziki wa asili na dansi la Mambo Safi
limeanza kambi rasmi leo katika ukumbi wa Harbous Klab kwa ajili ya kujiandaa na
sherehe za Mei mosi zitakazofanyika katika ukumbi wa Urafiki Club, Dar es
Salaam.
Kundi hilo ambalo sambamba na kutoa burudani hiyo pia
linajihusisha na kucheza sarakasi pamoja na Ngonjera litakaa kambi hiyo kwa muda
wa wiki moja ili kuweza kujiimarisha.
Akizungumza Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi wa SF group Camponies ltd ambayo ndio inasinamia kundi hilo Selina
Koka alisema katika kambi hiyo watakuwa wakifanya mazoezi katika burudani zote
wanazozitoa.
"kundi hili huwa linatoa burudani katika shughuli mbalimbali
za kiserikali na hii ni moja ya shughuli za kiserikali na ndio maana tumeamua
kuweza kambi ili kuweza kujiandaa vya kutosha kwa ajili ya kusheherekea siku
hiyo," alisema.
Aliongeza kuwa kundi hilo ambalo linajumla ya wanamuziki
22 linatarajia kuanza kutoa burudani kwa kila wiki katika ukumbi tofauti kama
zilivyobendi nyingine ili kuweza kutoa burudani zaidi.
Naye Mkurugenzi
mtendaji wa kundi hilo Phabbian Salvatory 'Super Phabby' alisema wanaliandaa
kundi hilo kutoa upinzani kwa bendi nyingine kongwe kama Extra bongo, Twanga na
nyinginezo ili kuweza kujiweka katika ramani nzuri ya muziki wa dansi hapa
nchini.
"hatutaki kuishia hapa tunataka kuwa kama bendi nyingine na hata
tuwashinde kwa kuwapa upinzani mkubwa ili kuweza kuwaonyesha uwezo wetu
tulionao," alisema.