Mkwasa kushoto, kulia Jamhuri Kihwelo |
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga
Stars, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 25 watakaoingia kambini kesho
(Aprili 20 mwaka huu) kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Zimbabwe
inayotarajiwa kuchezwa Aprili 28 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura amesema mchana huu kwamba mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Twiga
Stars kabla ya mechi ya mashindano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya
Ethiopia itakayochezwa Mei 26 mwaka huu jijini Addis Ababa kabla ya timu hizo
kurudiana jijini Dar es Salaam wiki mbili baadaye.
Wambura amesema baada ya kuripoti kambini jioni, wachezaji
hao watafanyiwa vipimo vya afya (medical examination) siku inayofuata (Aprili
21 mwaka huu) na kuanza mazoezi Aprili 22 mwaka huu. Kambi ya timu hizo itakuwa
kwenye hosteli za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Ruvu mkoani Pwani.
Wachezaji walioitwa ni Amina Ally kutoka Sekondari ya Lord
Baden, Asha Rashid, Aziza Mwadini (New Generation, Zanzibar), Etoe Mlenzi (JKT
Mbweni), Evelyne Sekikuto (Mburahati Queens), Fadhila Hamad (Uzuri Queens),
Fatuma Bashiri (Simba Queens), Fatuma Khatib (Mburahati Queens) na Fatuma
Mustafa (Sayari).
Wengine ni Fatuma Omari (Sayari), Hanifa Idd (Uzuri Queens),
Maimuna Said (JKT Mbweni), Mariam Aziz (Tanzanite), Mwajuma Abdallah
(Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba (Mburahati
Queens), Mwapewa Mtumwa (Sayari) na Rehema Abdul (Lord Baden).
Kikosi hicho pia kina akina Rukia Khamis (Sayari), Semeni
Abeid (Tanzanite), Siajabu Hassan (Evergreen), Sophia Mwasikili (Luleburgaz
Spor Kulubu, Uturuki), Veneranda Mtamo (Tanzanite), Zena Khamis (Mburahati
Queens) na Zena Said (Uzuri Queens).