KIUNGO Abou Diaby (pichani kulia) amesema matatizo ya majeruhi si kitu
akilinganisha na matatizo ambayo wachezaji wengine wamepitia.
Bunduki ya zamani Arsenal, Fabrice Muamba bado anaendelea na
tiba baada ya kupata matatizo ya moyo uwanjani akiichezea Bolton mwezi uliopita,
wakati beki wa kimataifa wa Ufaransa, Eric Abidal anatakiwa kwenda kufanyiwa
operesheni ya ini.
Diaby amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mara kwa mara ambayo
yamemfanya acheze mechi tatu msimu huu, lakini hana wasiwasi na anaamini mambo
yatakuwa sawa.
“Kusema ukweli kuna mazingira fulani ambayo unayafikiria juu
ya mustakabali wako, lakini ni muhimu kukubaliana nayo,” alisema.
“Wakati maumivu yanatokea, yanakuingia na huwezi kupata
ishu, ni vigumu sana. Kitu pekee unachoweza kufanya ni kuangalia mbele na kukubali.
“Kuna hali mbaya zaidi katika maisha kuliko inayonikabliT
mimi, hata kwenye soka, ukiangalia kilichowatokea Muamba au Abidal. Mimi, si
kitu.”