KOCHA wa Bolton, Owen Coyle amesema kwamba Fabrice Muamba anatembea
tena, yakiwa ni maendeleo mazuri juu ya matatizo yake ya moyo.
Muamba alizimia kwenye mechi ya Kombe la FA dhidi ya
Tottenham Machi 17, mwaka huu baada ya mapigo ya moyo wake kusimama kwa saa 78,
lakini kijana huyo wa umri wa miaka 23 anaendelea vizuri hivi sasa.
Kiungo huyo ambaye anatimiza miaka 24 Ijumaa, anamtia moyo
kocha wake kwa jinsi hali yake inavyoendelea, lakini Coyle ameonya bado anahitaji
muda mrefu zaidi ili kupona kabisa.
"Anapiga hatu, anazungumza na anatoa lile tabasamu pana
ambalo tunapenda kuliona. Anaelekea katika njia nzuri," alisema Coyle kuwaambia
Waandishi wa Habari.
Pamoja na kumkosa Muamba, ambaye ni mgonjwa, Bolton imeendelea
kufanya vizuri katika ligi, ikishinda mechi tatu mfululizo dhidi ya timu ambazo
zipo hatarini kushuka daraja na wao kufanikiwa kujiondoka kwenye eneo hilo.