Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz
Malinzi anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika kwa siku mbili
(Aprili 21 na 22 mwaka huu) kwenye ukumbi wa NSSF Waterfront jijini Dar es
Salaam.
Wajumbe wa mkutano huo watawasili jijini kesho (Aprili 20
mwaka huu) na watafikia kwenye hoteli ya Royal Valentino. Wajumbe wanatoka
katika vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu
ya Vodacom.
Mkutano huo utakaoanza saa 3 asubuhi utakuwa na ajenda kumi
na moja. Baadhi ya ajenda hizo ni hotuba ya Rais wa TFF, taarifa ya utendaji ya
mwaka 2011, bajeti ya mwaka 2012 na taarifa ya ukaguzi wa hesabu (audited
accounts).