Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
limeteua waamuzi kutoka Swaziland kuchezesha mechi ya kwanza ya 16 bora ya
Kombe la Shirikisho kati ya Simba na Al Ahly Shandy ya Sudan itakayochezwa
Aprili 29 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi hao wa mechi hiyo namba 71 ni Nhleko
Simanga Pritchard atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni Mbingo Petros
Mzikayifani na Sibandze Thulani. Mwamuzi wa mezani atakuwa Fakudze Mbongiseni
Elliot.
CAF pia imemteua Kayijuga Gaspard wa Rwanda kuwa
Kamishna wa mechi hiyo.