Kanumba |
MAMA wa marehemu Steven Kanumba,
ameanza kusumbuliwa na presha kiasi cha kulazimika kuwa chini ya uangalizi wa
daktari.
Dk. Nassor Matuzya kutoka
hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam ambaye amewahi kuwa Dakatri wa klabu
ya Yanga, enzi za kocha Mserbia, Profesa Dusan Savo Kondic ameiambia bongostaz
joni hii kwamba yupo kwa ajili ya kufuatilia hali ya Mama Kanumba.
“Mama anasumbuliwa na presha,
inapanda sana, lakini namtibu na kwa sasa anaendelea vizuri,”alisema Dk.
Matuzya.
Matuzya alisema Mama Kanumba leo
usiku atapelekwa hospitali ya Muhimbili, Dar es Salaam kuuona mwili wa mwanawe
kabla ya kuagwa na mazishi kesho.
Mama huyo aliyewasili jana
kutokea Bukoba, ameridhia mwanawe azikwe Dar es Salaam, ingawa baba wa msanii
huyo alipenda kijana wake azikwe karibu na kaburi la babu yake, Mzee Kanumba
huko Shinyanga.
Wakati huo huo: Mwanamitindo
Millenne Happiness Magesse ameongezwa kwenye kamati ya Mazishi. Millene ameonekana
tangu jana akiwajibika ipasavyo kwenye msiba huo.
Kanumba ataagwa kesho kuanzia
saa nne asubuhi, viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam na kuzikwa
kwenye makaburi ya Kinondoni.
Wakati huo huo: Watu wameendelea
kumiminika nyumbani kwa marehemu Sinza Vatican kutoa rambirambi na miongoni
mwao ni aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Imani Omar Madega.
Madega alifika kutoa salamu zake
za rambirambi na ubani kisha kuungana na waombolezaji wengine. Mwanamuziki mkongwe,
Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kiki’ naye alifika.
Every thing i hear about Kanumba is so sad and touching. Pole mama, Mungu atakupa nguvu, najua ni ngumu, lakini ni Mungu tu atakuwezesha, muombee mwanao, alale kwa amani.
ReplyDeletepoleni wote. Kanumba tulimpenda wote.