WEKUNDU WA Msimbazi, Simba SC wamewasili
Dar es Salaam alfajiri ya leo, wakitokea Algeria ambako waliitioa ES Setif ya
huko katika Kombe la Shirikisho kwa faida ya bao le ugenini baada ya sare ya
3-3.
Wapenzi na wanachama wa Simba
walimiminika kuilaki timu yao, lakini mapokezi hayakuwa makubwa kama
ilivyotarajiwa kutokana na muda na pili msiba wa mwigizaji Steven Kanumba.
Simba sasa imefuzu hatua ya 16
Bora ya Kombe la Shirikisho la Soka CAF, kwa licha ya kufungwa mabao 3-1 na ES
Setif kwenye Uwanja wa Mei 8, mjini Setif katika mchezo wa marudiano jana
usiku.
Shukrani kwake mshambuliaji wa
kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga bao la dakika za lala
salama wakati refa amekwishaonyesha dakika za majeruhi tano.
Katika mchezo huo, Simba ilipata
pigo mapema dakika ya 18 baada ya beki wake Juma Said Nyosso kutolewa nje kwa
kadi nyekundu kwa kucheza ‘rafu ya wazi’.
Hadi mapumziko, tayari Setif
walikuwa mbele kwa mabao 2-0 na mapema kipindi cha pili, wakapiga la tatu.
Mchezo wa kwanza Simba ilishinda
2-0 Dar es Salaam na sasa itamenyana na Al Ahly ya Sudan.
Simba sasa baada ya kuitoa ES
Setif imeingia hatua ya mwisho ya mchujo ambako itamenyana na ama El Ahly
Shandy ya Sudan na itaanzia nyumbani, mechi ya kwanza ikichezwa Aprili 29,
kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadaye Sudan.
Simba ikifanikiwa kuitoa El Ahly
Shandy, moja kwa moja itafuzu kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho
Afrika, ikiwa timu ya kwanza ya Tanzania kucheza hatua hiyo.
Tanzania imewahi kufikisha
katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa tu, mara mbili mwaka 1998 Yanga na
2003 Simba wenyewe.
Mwaka 2007 Yanga ilikaribia
kuingia hatua ya makundi ya Makundi ya Kombe la Shirikisho, lakini ikatolewa na
El Merreikh ya Sudan, wakati mwaka jana pia Simba ilikaribia kucheza hatua ya
makundi ya michuano hiyo, ikatolewa na Daring Club Motema Pembe ya DRC.
Kama wakifanikiwa kufika hatua
ya makundi ya michuano hiyo, Simba watapewa donge nono la dola za Kimarekani
150, 000, zaidi ya Sh. Sh Milioni 250,000 za Tanzania.
FEDHA ZINAZOWASUBIRI SIMBA SC:
NAFASI: KLABU TFF
Ubingwa $625 000 $35 000
Fainali $ 432 000 $ 30 000
Nafasi ya 2 kundini $ 239 000
$ 25 000
Nafasi ya 3 kundini $ 239 000
$ 20 000
Nafasi ya 4 kundini $ 150 000
$ 15 000