BAO la Mikel Arteta dakika za
majeruhi usiku huu limetosha kuipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester
City kwenye Uwanja wa Emirates, London.
Arteta alifunga bao hilo dakika
ya saba baada ya dakika 90 za kawaida za mchezo huo kutimia.
Sasa, matumaini ya Man City
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu yanaelekea kuota mbawa, kwani
imefikisha pengo la pointi nane dhidi ya vinara, Manchester United waliopo
kileleni.
City ilimpoteza Yaya Toure aliyeumia
mapema tu kwenye mchezo huo na bahati mbaya zaidi kwao mshambuliaji Mario
Balotelli alitolewa nje kwa kadi
nyekundu kwa kumchezea rafu Alex Song.
Arsenal sasa imefikisha pointi
61, baada ya kucheza mechi 32- inazidiwa pointi 10 na Man City iliyo nafasi ya
pili.
Mapema leo, mabao ya Wayne Rooney
kwa penalti dakika ya 15 na Paul Scholes dakika ya 68, yaliipa timu hiyo
ushindi wa 2-0 dhidi ya QPR na kuzidi kupaa kileleni.