MIYEYUSHO KUKIPIGA UINGEREZA APRILI 27

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) imetoa kibali kwa bondia wa kimataifa wa Tanzania Francis Miyeyusho (mwenye tisheti ya njano)kucheza pambano la ngumi nchini Uingereza. Miyeyusho atazipiga na bondia Luke Wilton wa Uingereza tarehe 27 mwezi huu katika hoteli ya Holiday Inn iliyo katika mtaa wa jijini Belfast, Ireland ya Kaskazini. Mpambabno huo ni wa kugombea mkanda wa kimataifa wa Masters katika uzito wa Super Fly.
Miyeyusho anatarajia kuondoika nchini tarehe 22 mwezi huu siku ya Jumapili na shirika la ndege la Uingereza (British Airways).
Francis Miyeyusho ni bondia wa kimataifa aliye kwenye viwango vya mashirikisho / vyama mbalimbali ya / vya ngumi duniani. Shirikisho la ngumi la Kimataifa IBF limemweka kwenye nafasi ya 5 katika orodha ya mabondia 15 bora wa mabara duniani.
Hii ni mara ya kwanza kwa Francis Miyeyusho kucheza nchini Uingereza na mabondia wa huko na anatagemea kuonyesha umahiri mkubwa katika mpambano huo.
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) inamtakia safari njema Miyeyusho katika safari yake ya kuitangaza Tanzania katika medani ya michezo ya kimataifa.
Ikumbukwe kwamba ni Ngumi za Kulipwa pekee ambazo zimekuwa zinaig’arisha na kuitangaza vyema Tanzania katika miaka ya karibuni.
Katika mpambano huo, wimbo wa Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia utapigwa mbele ya maelfu ya watanzamaji pamoja na mamilioni wengine ambao watakuwa wanaangalia kwenye luninga.
TPBC imeanzisha rasmi mkakati wa kutumia mchezo wa ngumi za kulipwa kuitangaza Tanzania kama sehemu salama ya kufikia kwa watalii na wawekezaji (destination market for tourism and direct investments) "Sports Tourism" kwa maana ya "Utalii wa Michezo"
Aidha tunamuombea mungu Miyeyusho aende salama na afanikiwe kurejea na mkanda wa International Masters nchini Tanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post