NEW YORK,
MAREKANI
NYOTA wa
mieleka kutoka chama cha mieleka duniani (WWE), Oscar Gutierrez ‘Rey Mysterio’ amesimamishwa
kwa muda wa siku 60 baada ya kufanya vurugu kwa mara ya pili katika mashindano
ya Talent Wellness Program.
Chama hicho
kimetoa taarifa yake mtandaoni kikisema kwamba, "kwa makubaliano na
waandaaji wa Talent Wellness Program, WWE imemsimamisha Rey Mysterio kuacha
kucheza kwa muda wa siku 60, kwa kufanya kosa la vurugu. "
Kwa mujibu
wa ripoti hiyo imesema mbabe huyo mwenye miaka 37, amechukuliwa uamuzi kutokana
na kurudia kosa hilo alilowahi kulifanya mwaka 2009.