Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba
na Moro United lililochezwa jana (Aprili 23 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam limeingiza sh. 28,688,000.
Jumla ya watazamaji 7,945
walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000,
sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji 6,946 kati ya hao walishuhudia mechi hiyo
kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada ya kuondoa gharama za
awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni
sh. 4,376,135.59 kila klabu ilipata sh. 4,919,009.32, uwanja sh. 1,454,286.44.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
sh. 1,454,286.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,058,414.58, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 727,143.22, Baraza
la Michezo la Taifa (BMT) sh. 145,428.64 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni
sh. 1,454,286.44.
Gharama za awali za mechi
zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa
mchezo sh. 10,000, mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna
na waamuzi sh. 80,000, gharama ya tiketi sh. 3,000,000, maandalizi ya uwanja
(pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000
na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Nayo mechi kati ya Villa
Squad na African Lyon iliyochezwa Aprili 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa Chamazi,
Dar es Salaam iliingiza sh. 496,000 ambapo kila klabu ilipata sh. 68,061.70
wakati watazamaji walioshuhudia mechi hiyo ni 469.
Vilevile mechi kati ya
Tanzania (Ngorongoro Heroes) na Sudan iliyochezwa Aprili 21 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam iliingiza sh. 9,717,000 kutokana na washabiki
2,562.