Fainali ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL)
iliyoshirikisha timu tisa imemalizika jana (Aprili 23 mwaka huu) kwenye Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro huku tatu zikifuzu kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
msimu wa 2012/2013 utakaonza Agosti mwaka huu.
Timu hizo ni Polisi Morogoro
iliyofikisha pointi 20 ikifuatiwa na Mgambo Shooting ya Tanga (15) na Tanzania
Prisons ya Mbeya iliyomaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi
14.
Nyingine zilizofuatia na
pointi zao kwenye mabano ni Polisi Dar es Salaam (13), Mbeya City Council (11),
Rhino Rangers ya Tabora (8), Mlale JKT ya Ruvuma (8), Polisi Tabora (6) na
Transit Camp ya Dar es Salaam (2).