Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Yanga
na Polisi Dodoma iliyochezwa (Aprili 22 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam ilishuhudiwa na watazamaji 1,635 na kuingiza sh.
5,666,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo
na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 864,305.08
kila klabu ilipata sh. 193,858.47, uwanja sh. 26,469.49.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) sh. 26,469.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 108,687.80. Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 13,234.75,
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 2,646.95 na asilimia 10 ya gharama za mechi
ni sh. 26,469.49.
Gharama za awali za mechi
zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa
mchezo sh. 10,000. Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna
na waamuzi sh. 160,000, gharama ya tiketi sh. 1,500,000, usafi na ulinzi kwa
uwanja sh. 1,500,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 1,000,000.
Kutokana na mechi hiyo
kuingiza kiasi kidogo baadhi ya gharama zililipwa nusu au kutolipwa kabisa na
kuacha madeni. Madeni hayo ni tiketi sh. 1,500,000, maandalizi ya uwanja (pitch
marking) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 850,000
na Wachina sh. 1,000,000.