Simba SC |
MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Simba
lililochezwa jana (Aprili 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
limeingiza sh. 30,095,000.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura amesema jumla ya watazamaji 8,362 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo
kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 15,000. Watazamaji
7,310 kati ya hao walishuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000.
Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18
ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,590,762.71 kila klabu
ilipata sh. 4,455,551.19, uwanja sh. 1,485,183.73.
TFF imepata Sh. 1,485,183.73, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa
wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 297,036.75 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Pwani (COREFA) sh. 297,036.75.
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 742,591.86,
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 148,518.37 na asilimia 10 ya gharama za
mechi ni sh. 1,485,183.73.
Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa
waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000 na nauli
ya ndani kwa mtathmini wa waamuzi sh. 10,000.
Mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna,
mtathmini wa waamuzi na waamuzi sh. 120,000, gharama ya tiketi sh. 3,750,000,
maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi
kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.
Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila
tiketi; kila klabu ilipata sh. 585,340 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) kilipata sh. 510,720.