Kocha mkuu wa Simba Milovan Cirkovic kushoto akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusaina na mechi yao na Al Ahli Shendi ya Sudan kesho, kulia ni mkuu wa msafara wa Shendi, Gamer Aldin Osman na kati ni ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura.
WAWAKILISHI
wa Tanzania katika kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF) Simba kesho wanashuka
katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kukipiga na Al Ahli Shendi ya Sudan
katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ya michuano hiyo.
Kocha
mkuu wa Simba Mserbia Milovan Cirkovic ameiambia mamapipiro blog kwamba kikosi chake kipo katika hali
nzuri na amekiandaa vema ili kiweze kushinda mchezo wa huo ili kujiweka katika
mazingira mazuri.
Hata
hivyo, Msebia huyo alishindwa kuahidi kama timu yake itaibuka na ushindi zaidi
ya kusisitiza kuwa amekiandaa vizuri kikosi chake na hasa kupitia michezo ya
ligi kuu soka Tanzania bara.
“Siwezi
kuahidi ushindi kesho lakini kikubwa ni kwamba nimekiandaa vema kikosi chake
hivyo ni matarajio yangu tutafanya vizuri katika mchezo wetu huo,”alisema.
Aidha,
Milovan aliongeza kuwa mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa na hasa
ikizingatiwa kuwa kila mmoja atahitaji kushinda ili kujiweka katika mazingira
mazuri kwenye mechi ya marudiano.
Naye
mkuu wa msafara wa Shendi, Gamer Aldin
Osman Siza, pamoja na kukiri kutoifahamu Simba, alisema wamejipanga vema
kuhakikisha wanashinda ugenini na hatimaye kwenda kumalizia kazi nyumbani
watakaporudiana.
Alisema
mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na wapiunzani wao nao kuhitaji
ushindi wa nyumbani hivyo dakika 90 ndizo zitaamua nani zaidi ya mwenzake.
Al
Ahly wanakutana na Simba baada ya kuitoa Ferroviario ya Msumbiji kwa jumla ya
mabao 3-0, huku Simba iliitoa Es Setif ya Algeria huku Simba ikibebwa na bao la
ugenini baada ya nyumbani kushinda 2-0 kabla ya kwenda kufungwa 3-1.
Mechi
hiyo itachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Swaziland Nhleko Simanga
Pritchard, Mbingo Petros Mzikayifani,Sibandze Thulani, Fakudze Mbongiseni Elliot na Kamishna wa
Kayijuga Gaspard wa Rwanda.
Mgeni
rasmi katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye
ambaye ni mmoja ya wadau wakubwa wa klabu hiyo.