WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe
la Shirikisho barani Afrika, (CAF) timu ya Simba wameanza kusaka mikanda ya
video ya wapinzani wao kwenye kombe hilo, Al Ahly Shandy ya Sudan.
Simba na Al Ahly Shandy
zitakwaana Aprili 29 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana leo toka
ndani ya klabu hiyo zinasema kwamba kazi ya kusaka kanda hizo wamempa mmoja ya
wachezaji aliyewahi kukipiga Simba aliyepo nje ya nchi.
Mmmoja ya viongozi wa Simba
aliuambia mtandao huu kwamba wameamua kusaka kanda hizo ili wafanyie kazi mbinu
za wapinzani wao hao.
Alisema wameamua kusaka kanda za
wapinzani hao kutokana na kutoifahamu vema timu hiyo hivyo wanaamini kanda hizo
zitawasaidia kwa kiasi kikubwa.
Tayari kikosi cha Simba
kimeingia kambini jioni ya leo katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni
jijini Dar es salaam kujiandaa pia na michezo yake ya ligi kuu soka Tanzania
bara ambapo jumapili hii itakwaana na maafande wa Ruvu Shooting katika uwanja
wa Taifa.