Shujaa Drogba |
BEKI la kati, John Terry amesema anajiamini Chelsea itatinga
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Barcelona 1-0 kwenye Uwanja
wa Stamford Bridge katika Nusu Fainali ya kwanza usiku wa jana.
Bao la Drogba mwishoni mwa kipindi cha kwanza lilitosha kuipa
timu ya London ushindi na Nahodha huyo Chelsea anaipongeza timu yake kwa
jitihada kubwa walizoonyesha kwenye mechi na Barcelona.
“Nafikiri tulitulia usiku huu (jana), tulizidiwa kumiliki
mpira mwanzoni, sifikiri kama tuliugusa katika dakika 10 hadi 15 za mwanzo,” alisema
Terry katika taarifa iliyoifikia bongostaz.
“Kawaida wao ni timu babu kubwa. Tulitakiwa kutulia haswa. Ilikuwa
babu kubwa, kujituma kwa kila mmoja bila kuchoka.”
Licha ya bao la Drogba, lakini wageni walipoteza nafasi
zaidi ya tatu za wazi za kufunga na Terry amempongeza sana Nahodha wa Ivory
Coast kwa bao lake.
“Ni hodari, ndivyo anavyokuwa katika mechi kuvwa kama hizi, ulimuona
Jumapili dhidi ya Tottenham Uwanja wa Wembley,”alisema Terry.
“Anakabiliana na mabeki bora duniani na anawaacha. Kuna wakati
alipagwa, lakini aliimudu mechi vizuri.”
Chelsea sasa itasafiri hadi Uwanja wa Camp Nou wiki ijayo
huku Nahodha wake, akiwa mwenye kujiamini kwamba watacheza fainali msimu huu
dhidi ya ama Real Madrid au Bayern Munich.
“Nafikiri dhahiri itakuwa mechi ngumu huko, tuliokoa mabao
kadhaa ya wazi kwenye mstari wa lango letu, dhahiri watapata nafasi huko kwenye
Uwanja wenye eneo kubwa la kuchezea, wao ni wazuri,”alisema.
“Tumeonyesha tunawaheshimu usiku huu (jana), lakini hatuko
kwenye himaya yao na tutafanya biashara.”
Drogba, wakati huo huo amesema anafikiri The Blues wamejifunza
kutokana na mwaka 2009 walipotolewa na Barcelona na amefurahishwa na matokeo ya
jana.
“Nafikiri tumejifunza [kutokana na makosa ya kufungwa 2009].
Tumeimarika ndani ya miaka mitatu, kwa sababu hatukufungwa bao (la nyumbani),” alisema.
“Tuna furaha na matokeo haya. Ni mazuri, 1-0 nyumbani, ni
matokeo mazuri. Tutakwenda huko na kujaribu kufunga bao lingine na kufuzu,”amesema
Drogba kama tunavyomnukuu bongostaz.blogspot.com.