Wachezaji 10 wamepita katika mchakato wa kusaka vipaji kwa
chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa
Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania
(TFF) uliofanyika kuanzia Mei 21-26 mwaka huu.
Watoto zaidi ya 1,500 walishiriki katika mchakato huo
uliokuwa chini ya mng’amua vipaji (scout) Gisbert Xavier kutoka Hispania, na
ulifanyika katika vituo vya Morogoro, Bagamoyo mkoani Pwani, na Kawe, Makongo,
Magomeni, Tabata, Kitunda, Tandika, Ukonga na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
kwa Dar es Salaam.
Kituo cha Morogoro amechaguliwa Karim Hussein wa Shule ya
Sekondari Nanenane, kituo cha Magomeni ni Joseph Mushi wa Shule ya Msingi
Mwalimu Nyerere wakati kituo cha Tabata ni Martin Tangazi.
Tandika ni Ismail Ngakonda (Shule ya Sekondari Uwanja wa
Ndege), Kitunda ni Nicholas Lauteri (Shule ya Sekondari Ulongoni), Omari Mbwai
(Shule ya Sekondari Msongola) na Hamad Omari (Shule ya Sekondari Ulongoni).
Kituo cha Ukonga ni James Msuva (Shule ya Sekondari Makongo)
wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ni Adolf Mtasigwa (Shule ya Sekondari
Loyola) na Ally Hatibu (Shule ya Sekondari Kurasini).
Mng’amuzi huyo wa vipaji anatarajia kufanya mchujo wa mwingine
kabla ya chipukizi hao kwenda Nairobi ,
Kenya kwenye
mchujo wa mwisho baada ya kambi ya ya siku nne kuanzia Juni 5-9 mwaka huu.