KOCHA wa Taifa Stars Kim Poulsen amekana kupendelea katika uteuzi wa wachezaji wa kikosi hicho na kusema kwamba alichagua wachezaji
kutokana uwezo na sifa walizonazo na si kuangalia ni mchezaji wa timu gani.
Alisema nashangazwa na maalalamiko ya baadhi ya wadau wa soka ambao wamekuwa wakielekeza shutuma hizo ambazo hazina ukweli wowote.
Baadhi ya wadau walimekuwa wakimlalamikia kocha huyo kutokana na kuchagua nyota wengi kwenye kikosi hicho wakitokea klabu ya Simba huku mahasimu wao Yanga, akiteua mchezaji mmoja tu.
Aliongeza kuwa kikosi chake ambacho kinajiandaa na mchezo wake wa kuwania kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast kitaenda bila ya nyota wake Nurdin Bakari na Thomas Ulimwenguni ambao walipata
majeruhi wakati wa mazoezi yao na kusema kuwa
watabaki wakijinoa kabla ya kuungana na wenzao watakaporudi ili kujiandaa.
Akizungumzia mchezo wao dhidi
ya Ivory Coast utakaopigwa juni 2 huko Abdjan, Paulsen alisema kikosi chake kinaiheshimu kutokana na kuwa na
wachezaji nyota wengi wenye uwezo kisoka
kwa ambao wanacheza ligi za ulaya wakiwemo Didier Dragba, Solomon Kalou, Yaya Toure, Kolo
Toure na wengineo.
Alisema pamoja na hilo hawaiogopi zaidi ya
kuwataka wachezaji wa Stars kutambua hawana tofauti na Ivory Cost isipokuwa ni
mbinu tu za hapa na pale ambazo anaamini kwa uwezo walichonacho wachezaji wa
Stars wanaweza kushinda.na
mechi yao dhidi ya Gambia .
Wachezaji wengine waliopo
Stars ni pamoja na makipa; Juma Kaseja
(Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki:
Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto
Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe
(Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto
(Simba), Salum Abubakar (Azam), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa
Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo
(JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana
Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ), Ramadhan Singano
(Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).