Na Mbaruku Yusuph, Tanga
KLABU ya Coastal Union iko
katika maandalizi kabambe ya kujiandaa na mechi yao ya kumalizia msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara
dhidi ya Toto Africa inayotarajiwa kupigwa dimba la Mkwakwani jijini hapa.
Akizungumza jijini hapa juzi,
Kocha Mkuu wa Wagosi wa Kaya, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, alisema wameamua kuanza
maandalizi ili kuhakikisha wanachukua pointi zote tatu muhimu kwenye mechi
hiyo.
Kihwelu alisema kutokana
na uimara wa kikosi chake ambacho kimekuwa tishio kwa baadhi ya timu kongwe
zinazoshiriki ligi hiyo, wana imani kubwa ya kuibuka na ushindi wa kishindo
wakiwa nyumbani.
“Ninachoweza kusema ni
kuwa mechi hiyo haitusumbui akili, kwani tuna imani kubwa na kikosi chetu
kuweza kushinda siku hiyo,” alisema Julio.
Kocha huyo aliwataka
mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo, ili kuwapa hamasa wachezaji
kufanya vizuri.