Mobondia wa timu ya taifa waTanzania Selemani
Kidunda 69 kgs welter weight na Emillian Patrick
56 kgs bantam weight wamesonga mbele katika mashindano ya
kufuzu kuelekea katika kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika London
Uingereza,katika mashindano yaliyoanza tarehe 28/4-5/5/2012 Casablanca
Morocco.
Mabondia hao wamefika hatua hiyo baada ya kushinda mapambano
yao ya awali kwa seleman Kidunda kumshinda Kab Thiam wa Senegal kwa RSC na
Emillian Patrick kumshinda Tewodros Tilahun wa Ethiopia.
Mabondia hao sasa wamefika katika hatua ya robo fainali
ambapo ni jumla wa mabondia nane waliofikia hatua hiyo na idadi inayotakiwa
kufuzu ni mabondia sita kwa kila uzito.
Mabondia hao kesho tarehe 2/5/2012 watapanda ulingoni kwa
Emillian Patrick kucheza na Isaac Dogboe wa Ghana na
Seleman Kidunda atacheza na Mehdi Khalsi wa Morocco .
Endapo watashinda watakuwa wameingia hatua ya nusu fainali na
tayari watakuwa wamefikia hatua ya kupata medali ya shaba .
Tanzania ilipeleka jumla ya wachezaji wanne na viongozi
wawili wachezaji wawili Victor Njaiti na Abdalah Kassim walitolewa katika hatua
za
awali.
viongozi walioambatana na timu ni Michael Changarawe na Remmy Ngabo.
Aidha kesho kutafanyika mkutano mkuu wa Shirikisho la ngumi
la Afrika (AFBC) Tanzania katika mkutano huo itawakilishwa na makamo wa Rais wa
BFT Michael Changarawe
Kwa niaba ya BFT tunawaomba watanzania wote kila mmoja kwa
imani yake kuwaombea ili washinde na wafuzu kushiriki mashindano
ya Olimpiki kwa kuzingatia kuwa kwa upande wa ngumi tulishiriki olimpiki kwa
mara ya mwisho mwaka 1996 Atlanta.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu (BFT)