Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
linatoa pongezi kwa timu ya Simba kwa ushindi wa mabao 3-0 ambao iliupata juzi
(Aprili 29 mwaka huu) dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan katika mechi ya Kombe la
Shirikisho iliyochezwa Dar es Salaam.
Ushindi huo umetokana na
ushirikiano uliopo kuanzia kwa wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama
wa klabu hiyo na Watanzania kwa ujumla.
Ni imani ya TFF kuwa Simba
haijabweteka kwa ushindi huo na badala yake sasa inajipanga kwa ajili ya mechi
ya marudiano itakayochezwa nchini Sudan ili kuondoa Al Ahly Shandy kwenye
michuano hiyo na kusonga mbele.
TFF kama kawaida itaendelea
kutoa ushirikiano kwa Simba ili kuhakikisha inafika mbali kwenye mashindano
hayo, na ikiwezekana kuandikika historia ya kuwa timu ya kwanza ya Tanzania
kutwaa Kombe la Shirikisho.