KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango wa Simba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tazara, Dar es Salaam.
Mafisango amefariki kwa ajali ya gari akiwa anarejea nyumbani kwake, kutoka disko na kwa sasa mwili wke upo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Meneja wa Simba SC, Nico Njohole amethibitisha kifo cha mchezaji huyo na amesema hilo ni pigo kubwa kwa klabu hiyo.
Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 Rwanda na kabla ya Tanzania alichezea APR ya Rwanda. Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea SImba ilikuwsa dhidi ya Al Ahly Shandy Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.
Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange Kaburu alisema kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao. Poleni wana Simba wote, pole kwa ndugu, jamaa na familia ya Mafisango. Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele. Amin. Mungu iweke pema peponi Roho ya Marehemu. TAARIFA ZAIDI ZINAKUJA:
POLENI WANYAMA KWA KUONDOKEWA NA PATRIC,BUT NAJUA LAZIMA ITAKUA ALIKUA ANAENDESHA AKIWA AMELEWA KWA KUWA JAMAA ALIKUA MNYWAJI SANA WA POMBE,HII TUICHUKULIE KAMA CHALLENGE,TUSITUMIE VYOMBO VYA MOTO TUKIWA TUMEKUNYWA POMBE.
ReplyDeleteInasikitisha, lakini kifo kimeumbiwa viumbe hai, katangulia sisi tu nyuma yake Dina, ila meneja wa Simba sio Nico Njohole, bali Nico Nyagawa!
ReplyDeletePOLENI WANSIMBA ILA TUJITAIDI KUTOA ELIMU KWA WACHEZAJI WETU WAFANYE VITU KWA KIASI. INGAWAJE SIKU YAKE IMEFIKA.
ReplyDelete