RAGE-TULIFUNGWA KIHALALI SUDAN

SIMBA imesema kutolewa kwake kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF) ni sehemu ya mchezo na hakuna haja ya kuelekeza shutuma kwa mchezaji yoyote. Wekundu hao wa Msimbazi walitolewa na Al Ahli Shandi ya Sudan jumapili iliyopita kwa penalti 9-8, baada ya timu hizo kumaliza kwa sare ya mabao 3-3. Mwenyekiti wa Simba Al Hajj Ismail Aden Rage ameiambia mamapipiro blog kwamba, Watanzania waliouona mchezo huo kupitia katika televisheni hivyo wanafahamu kilichotokea uwanjani Alisema mabao mawili ya haraka waliyofungwa ndiyo yaliwachangaya zaidi wachezaji wake na kujikuta wakipoiteza mwelekeo kabisa wa mchezo huo. Kuhusiana na taarifa za hujuma walizokumbana nazo pindi walipowasili Sudan kuwa huenda zilichangia kufungwa kwao, Rage alisema hakubaliani na hali hiyo kwani baada ya kuona hali hiyo waliwajenga wachezaji wao kisaikolojia. Rage pia aliwapongeza wachezaji wa Simba kutokana na umahiri wao katika kuhakikisha wanashinda mchezo huo lakini bahati haikuwa yao siku hiyo. Katika hatua nyingine, Rage alisema wanatarajia kufanya sherehe maalum ya kujipongeza kwa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2011/2012 zitakazofanyika Mei 27 kwenye ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Rage alisema kupitia sherehe hizo zitakazohudhuriwa na wadau pamoja na mashabiki mbalimbali wa Simba kutakuwa na burudani za muziki wa bendi na ile ya kizazi kipya.

1 Comments

  1. Kweli kabisa siyekubali kushindwa sio mshindani, turudi nyumbani kwenye `chandimu chetu'

    ReplyDelete
Previous Post Next Post