WAREMBO watakaoshiriki shindano la Miss Dar Intercollege
2012 kesho wanatarajiwa kuanza mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo kwenye
hoteli ya Lamada, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano
hilo Dina Ismail alisema jana kwamba warembo hao watatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na
Time, pamoja na Ustawi wa Jamii.
“Kesho (leo) tutaanza mazoezi yetu pale Lamada ambapo
warembo kutoka vyuo vinne wataanza kujinoa…wiki ijayo huenda tukaongeza
washiriki wengine ambao watatoa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambao
wanafanya shindano lao mwishoni mwa wiki hii,”alisema.
Alisema kuwa warembo hao watakuwa chini ya ukufunzi wa mrembo aliyepata kushiriki shindano hilo , Rose John, huku kwa
upande wa shoo watanolewa na Bob Rich.
Dina aliwataja wadhamini waliojitokeza mpaka sasa ni pamoja
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s, Lamada Hotel, Ndege
Insurance, na Dodoma Wine, huku akiomba
makampuni mengine kujitokeza kudhamini shindano hilo litakalofanyika mwezi
ujao.