BARAZA la wazee la klabu ya Yanga
limesikitishwa na kauli za kejeli na zenye kuwadhalilisha alizozitoa mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd
Nchunga juzi, hivyo kuanzia sasa wamemwachia aendelee na timu hiyo.
Hatua hiyo inafuatia Nchunga kudai kuwa wazee hao
walikurupuka na hawezi kukabidhi kwa wahuni, pia sehemu ambapo hana uhakika na
usalama, huku akihofu timu hiyo kuhudumiwa na wauza dawa za kulevya.
Wakizungumza na mamapipiro blog leo asubuhi wazee hao
wakiongozwa na katibu wao Ibrahim Akilimali walisema kwamba hawakukupupuka
kutangaza kuichukua timu bali walikubaliana na Nchunga, lakini wanashangaa
baadaye kuwageuka.
“Hatukukurupuka kuongea vile, ilikuwa ni ridhaa ya
Nchunga, tulikuwa sahihi kutokana na mapenzi yetu na timu, pamoja na kuwa
uongozi ndio una haki tuliikubaliana kuichukua timu kwa lengo la kuhakikisha
inaifunga Simba, tunafanya usajili wa uhakika na kurejesha nidhamu,”alisema.
“Ni ajabu kwa Nchunga kututamkia sisi wauza unga,
inamaana mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, Seif Ahmed, Abdallah Binkleb na
Yusuf Manji ni wauza unga?
...hivi Nchunga anajua umuhimu wa hawa watu ndani ya
Yanga,tena kwa mshangao mkubwa amediriki hata kutuma watu wamzuie kuingia
klabuni mzee Kitundu (Jabir)ambaye
alishiriki kuijenga klabu,”alisema Mzee Akilimali.
Naye mjumbe wa baraza hilo, Yussuf Mzimba pamoja
kusikitishwa na kauli za Nchunga, alisema Yanga ina wenyewe na kwamba ukifuga
kuku wengi lazima utapata aliye kisirani ambao wanajifanya wanajua kumbe si
lolote.
“Tunataka serikali iangali watu kama hawa, Nchunga
hawezi kutukana watu kama kina mama Karume, inaonekana klabu imemshinda kwani
aliingia madarakani kwa bahati tu na matokeo yake kaleta mgawanyiko badala ya
umoja”,alisema mzee Bilal Chakupewa.
Aidha Mzee Chakupewa aliongeza kwamba hata kama
wakiifunga Simba jumamosi Nchunga ni lazima aondolewe madarakani kutokana na
udhaifu aliouonyesha kwenye uongozi wake na kuifikisha Yanga mahala pabaya.