WAKATI mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF)
baina ya Simba na Al Ahli Shendi ya Sudan ukiingiza shilingi milioni 216,kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi yake ya mchezo wake wa mwisho wa ligi kuu soka Tanzania
Bara dhidi ya Yanga utakaopigwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza na mamapipiro blog kwa simu kutoka Visiwani Zanzibar ambapo
timu imepiga kambi, msemaji wa Simba Ezeckiel Kamwaga alisema kwamba kikosi chao ambacho kimepiga
kambi eneo la Mbweni kipo katika hali nzuri na kinafanya mazoezi katika uwanja
wa Fuoni.
Aliongeza kuwa wamepania kushinda mchezo huo ili kulipiza
kisasi cha kufungwa bao 1-0 na mahasimu hao katika mzunguko wa kwanza wa ligi
hiyo ambayo Simba inaongoza kwa pouinti 59 ikifuatiwa na Azam Fc yenye pointi
56 na Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 46.