Warembo watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya
Miss East Africa mwaka huu wameanza kutangazwa.
Mrembo wa kwanza kupatikana ni Miss Rahwa Afework (22)
kutoka Nchini Eritrea ambae
aliwashinda wenzake waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Eritrea katika
mashindano hayo.
Miss Rahwa Afework mwenye urefu wa 1.73m anasomea mambo ya
Fashion design Nchini Eritrea .
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika
tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha
Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea,
Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na
Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam