WAWAKILISHI wa Tanzania
katika kombe barani Afrika (CAF) Simba
inaondoka nchini mchana wa kesho kwenda Sudan huku ikiwaacha nyota wake
kadhaa wakiwemo Juma Nyoso na Ulimboka Mwakingwe, Nassoro Said ‘Chollo’
imefahjamika.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia mamapipiro blog kwamba wachezaji hao wameachwa kutokana na sababu mbalimbali, huku wale
waliomo katia msafara humo wakiwa na ari kubwa ya mchezo huo.
Alisema kuwea msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji 20 na
viongozi watano wataenda huko tayari kwa
mchezo wao wa marudiana na Al Ahli Shandi ya huko utakaopigwa jumapili hii.
Alisema msafara huo utakaokuwa chini mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Hussein Mwamba utaondoka kwa
ndege ya Shirika la Kenya
(KQ), ambapo wachezaji wote watakaokwenda huko wapo katika hali nzuri.
Aliongeza kuwa uongozi unamatarajio makubwa ya timu hiyo
kusonga mbele kutokana na matayarisho waliyoyafanya huku wakichagizwa zaidi na
kutwaa ybingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara iliyomalizika jumapili iliyopita.
Hata hivyo Kaburu alisema wataenda Sudan wakiwa na
tahadhari kubwa kutokana na ukweli kwamba wapinzani wao watafanya kila njia
kutokana na uenyeji wao kuhakikisha wanatumia vema uwanja wa nyumbani.
“Kama mnavyojua tuliwafunga Shendi tulivyocheza naop sasa
sidhanui kama watabweteka na kutaka kufungwa
kirahisi, kwa hali hiyo tumejipanga ipasavy kukabiliana na hali yoyote
tutakayokutana nayo huko ili kuweza kushinda,”alisema Kaburu.
Katika mchezo wa awali uliopigwa nchini wiki iliyopita Simba
iliifunga Shendi mabao 3-0 katika mchezo hivyo inahitaji kulinda ushindi wake
kwa namna moja ama nyingine ili kusonga mbele.