USAJILI AIRTEL RISING STARS MWISHO JUMATANO


Participants to a one-day Airtel Rising Stars directive seminar take part in a brief warm up during a one-day directive seminar held in Dar es Salaam over the weekend to guide school sports masters and regional football administrators on rules and regulations governing the U-17 Airtel Rising Stars tournament.



Usajili wa wachezaji kwa ajili ya michuano ya Airtel Rising Stars  2012 inatarajiwa kufikia tamati Jumatano, Mei 23 kwa mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha, Mbeya na Aruhsa. Jumla ya timu 24 zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ngazi ya miaka na hatimaye ngazi ya Taifa itakayofanyika mwezi Julai Jijini Dar es Salaam
Mikoa shiriki ilichanguliwa kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano ya Taifa ya Shule za Sekondari (UMISSETA) iliyoisha hivi karibuni. Uzinduzi rasmi wa Airtel Rising Stars 2012 ulifanyika hivi karibuni chini ya mchezaji wa zamani wa Manchester United ya Uingereza, Quinton Fortune kwenye Hoteli ya Sea Cliff, Dar es Salaam.
Michuano ya Airtel Rising Stars 2012 ina umuhimu wa kipekee kwa kuwa timu sita za wasichana zitashiriki kwenye ngazi ya Taifa. Akiongea kuhusu wasichana kushiriki kwenye michuano hii, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Cheikh Sarr alisema, ‘Airtel imeamua kujumuisha wasichana kwenye michuano hii kuwapa nafasi ya kuendeleza vipaji vyao na pia kuipa Timu ya Taifa ya wanawake ya Twiga Stars wasaa wa kupata vipaji vipya.
Wakati wavulana wakitarajiwa kushindana kuanzia ngazi ya mkoa ili kuchanguliwa kupata nafasi ya kucheza Taifa, timu moja ya wasichana kutoka kila mkoa itashiriki moja kwa moja fainali za Taifa na hivyo kufanya timu 12 kushiriki, ngazi hii, sita wavulana na sita wasichana.       
Akizungumzia juu ya Airtel Tanzania kuwekeza kwenye soka, Cheikh Sarr alisema ‘ Tunajisikia furaha kukuza vipaji vidogo kuanzia ngazi ya chini kabisa, huu ndio muda kila mtu alikuwa akiisubiri.’ Ni muda muafaka kwa Tanzania kuzalisha stars wake – aliongeza Sarr.
Michuano ya ARS ngazi ya mkoa inarajiwa kuanza Mei 25, huku Dar es Salaam ikiwa na timu sita kutoka Kinondoni, Ilala na Temeke. Shule hizo ni Twiga, Goba na Makongo Sekondari (Kinondoni) Mbande, Kurasini na Kiravi Sekondari (Temeke) huku Ilala ikiwakilisha na Airwing, Benjamin Mkapa na Msongola Sekondari.
Shule zingine zitakazoshiriki kwenye michuano hii ni Southern Highland Sekondari, Mbeya High na Wenda Sekondari (Mbeya), Lindi Sekondari, Mpunyule na Ngowe Sekondari (Lindi) huku Arusha ikiwakilisha na Sinoni Sekondari, Kaloleni na Bishop Durning Sekondari.
Michuano wa Airtel Rising Stars ni mpango kambambe kwa Afrika nzima ambao ni wa kutafuta na kukuza vipaji vya soka vinavyochipukia kwa wavulana na wasichana wenye miaka chini ya kumi na saba ambao watapata muda wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na wataalamu wa mpira wa miguu ambao watawapa mafunzo zaidi na kupata nafasi ya kukuza vipaji vyao.
Airtel Rising Stars ni ushirikiano kati ya Airtel na klabu ya Uingereza ya Manchester United ya kukuza vipaji vya soka barani Afrika. Mwaka jana, Klabu ya Manchester United ilitoa walimu wake wa soka ya vijana kuendesha kliniki ya soka ya Kimataifa ambazo kliniki hizo zilifanyika Tanzania, Afrika Kusini na Gabon.
Kliniki ingine kama hiyo itafanyika Nairobi, mwezi wa Agosti mwaka huu huku ikitanguliwa na michuano ya kimataifa itakayohisishwa timu bingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars.


Post a Comment

Previous Post Next Post