WAKATI Kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars' kiliingia kambini jana, wachezaji wengi wa timu hiyo wameitia wito wa kocha mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen leo kwa kuripoti.
Stars ilianza mazoezi jana kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast Juni 26 ambapo Mei 26 itacheza kwanza na Malawi. Nyioni na Kelvin Yondan. itacheza mechi ya kirafiki na Malawi.
hata hivyo wachezaji kama Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ambao wanacheza soka la kulikupwa katika klabu ya TP Mazemya Congo bado hawajaripoti.
Mbali na hao wachezaji wengine ambao hawakuripoti hadi jana mchana ni pamoja na Shaban Dihjile,Erasto Nyoni na Kelvin Yondan.
Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).
Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.