KAMATI
ya uchaguzi ya klabu ya Yanga imetangaza rasmi majina ya wagombea katika
uchaguzi mdogo wa Julai 15, huku ikionya atakayewasilisha pingamizi feki dhidi
ya mgombea, atafungiwa na kulimwa faini.
Kwa
mujibu wa Katibu wa Kamati hiyo, Francis Kaswahili, mwanachama atakayewasilisha
pingamizi bila vielelezo, atafungiwa na soka kwa miaka miwili na faini sh
500,000.
Kaswahili
alisema, wameamua kuweka tahadhari hiyo kutokana na kasumba iliyojengeka kwa baadhi
ya wanachama kufanya hivyo kwa chuki zao binafsi.
Alisema,
wakati mwanachama wa aina hiyo akifanya
mzawa
kwa kuleta tuhuma zisizo na ushahidi, bado
kamati
hupoteza muda wake kuzishughulikia.
Alisema,
ingawa hiyo ni sehemu ya kazi yao ,
lakini ni wajibu
wa
mwanachama kuwasilisha pingamizi akijiridhisha kuwa,
ana
vielelezo vya kutosha dhidi ya madai yake.
“Hatukatai,
mwanachama ana haki ya kumwekea pingamizi mgombea yoyote, lakini pingamizi liwe
limejitosheleza kwa maana ya ushahidi wa vielelezo,” alisema Kaswahili na
kuongeza:
“Tunatoa
tahadhari kwa wanachama mwenye nia ya kuwasilisha pingamizi, afanye hivyo kwa
vielelezi, si kwa
chuki
binafsi na fitna tu dhidi mgombea, atakayebainika ataadhibiwa,” alisema.
Kuhusu
upitiaji wa fomu za wagombea, Kaswahili alisema
limekamilika
na keshokutwa watabandika ubaoni majina
ya
waliopitishwa kutoa nafasi kwa wenye mapingamizi.
Alisema,
mgombea Abdallah Sharia wa Zanzibar ,
amepewa muda wa kuwasilisha vyeti huku Mohammed Mbaraka akishindwa kuwasilisha cheti
cha kidato cha nne.
Alisema
kwa nafasi ya Mwenyekiti inayowaniwa na wagombea wanne, wamepita wote ambao ni
Yusuf Manji, John Jambele, Edgar Chibura na Sarah Ramadhan.
Waliopita
nafasi ya makamu, ni Ayoub Nyenzi, Clement Sanga, Yono Kevela na Ally Mayai
Tembele, nyota wa zamani wa Yanga na timu ya soka ya Tanzania , Taifa Stars.
Wajumbe
waliopita ni Lameck Nyambaya, Ramadhani Kampira, Mohamed Mbaraka ‘Binkleb’,
Ramadhan Said,
Edgar
Fongo, Ahmed Gao na Beda Tindwa, Jumanne.
Wengine
ni Mwamenywa, George Manyama, Gadeuncius Ishengoma, Aron Nyanda, Omary Ndula na
Shaban Katwila.
Wamo
pia Justine Baruti, Jamal Kisongo, Peter Haule,
na Stanley Kevela ‘Yono’ ambaye pia anagombea nafasi ya Makamu
Mwenyekiti.
Kaswahili
alisema milango ya kuwasilisha pingamizi dhidi
ya
wagombea, itafunguliwa kuanzia Juni 14-18, baada ya
hapo
kamati yao na ile ya Shirikisho la soka Tanzania
(TFF), zitapitia.
Uchaguzi
unafanyika kuziba nafasi ya Mwenyekiti, Makamu
na
nne za ujumbe wa Kamati ya Utendaji baada ya wahusika kujiuzulu na kufariki
dunia.
Wakati
Mwenyekiti Lloyd Nchunga, Makamu Devis Mosha na wajumbe watatu wakijiuzulu kwa
nyakati na sababu tofauti, mjumbe
Thenest Rutashoborwa alifariki dunia hivi karibuni.
Nchunga
na wajumbe watatu, walijiuzulu mwezi uliopita kutokana na presha ya wazee chini
ya Ibrahim Akilimali
na
Bakili Makele kwa upande wa vijana.