MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Simba, Mzambia Felix Mumba Sunzu ameondoka nchini leo kuelekea jijini Lubumbashi, DRC
kuhudhuria msiba wa dada yake ambaye alifariki dunia juzi jioni nchini
humo.
Dada huyo alikuwa amekwenda kumtembelea mdogo wa Sunzu, Stopila,
ambaye anachezea klabu ya soka ya TP Mazembe siku sita zilizopita lakini
akakumbwa na umauti kutokana na ugonjwa wa Malaria iliyopanda kichwani
(Cerebral Malaria).
Uongozi wa Simba umetoa pole kwa familia ya Sunzu pamoja na
kufanikisha kuondoka kwa haraka kwa mchezaji huyo ili akaungane na
familia yake.
Sunzu atarejea nchini baada ya kumaliza maziko na klabu ya Simba
inaomba vyombo vya habari na wadau wengine kumpa nafasi ya kuomboleza
msiba huu mzito kwake binafsi, kwa familia yake na Simba.
Mola na aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen