WASANII WASHAURIWA KUJIIMARISHA KITAALUMA



Mkufunzi wa masuala ya aundaaji wa Filamu kutoka taasisis ya Sanaa na uandishi wa Habari (IAMCO) Ngalimecha Ngahyoma, akizungumza jambo katika Jukwaa la Sanaa, kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz) Hassan Bumbuli na kushoto ni Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego

Na Mwandishi Wetu
Wasanii wa nchini wametakiwa kujiimarisha katika masuala ya taaaluma ili waweze kufanya kazi zenye ubora na zinazokidhi mahitaji  ya soko la ndani na nje ya nchini.

Akizungumza katika Jukwaa la Sanaa jana, mkufunzi wa masuala ya uandaaji wa filamu hapa nchini Ngalimecha Ngahyoma amesema kumekuwa na matatizo mengi katika uandaaji wa kazi za filamu hapa nchini kutokana na wasanii kutokuelewa misingi ya uandaaji wa filamu.

“Kuna maeneo ya msingi ambayo yanahitaji watu kubobea ili kuyafanya kwa utimilifu, na hakuna njia ya mkato ni lazima kuyapata shuleni kwa maana lazima mtu ufundishwe. Wasanii wengi wanatumia vipaji vyao, lakini matokeo ya kufanya mambo kwa vipaji ndiyo haya ambayo yanatupa filamu zenye matatizo katika maeneo mbalimbali,” alisema.

Alisema ni muhimu kwa wasanii kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake kuanza kuandaa kazi kitaalamu ili kufanya kazi zilizobora na kwamba ni vyema kutumia wataalam katika maeneo yote yanayohitaji utalaam badala ya mtu mmoja kufanya kazi zote.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ghonche Materego, amesema suala la taaluma alikwepeki katika kutengeneza kazi zenye ubora na kuwasisitiza wasanii kujiunga na vyuo kupata utaalam katika fani zao.
 

Post a Comment

Previous Post Next Post