HATIMAYE kamati ya
Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF imewaidhinisha
kuichezea Yanga mabeki
Mbuyu Twite na Kevin Yondan ambao waliwekewa pingamizi na mahasimu wao
nchini, Simba .
Katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi jana, pamoja na
maamuzi hayo Yanga wametakiwa kuilipa Simba dola 32,000 ambazo walimpa Twite ili ajiunge nao kabla ya Yanga kuingilia
kati na kumsajili.