SERIKALI imesema
itakuwa vema kama vazi la Taifa likavaliwa rasmi katika maadhimisho ya miaka 51
ya Uhuru wa Tanganyika itakayoadhimishwa tarehe 9 Desemba, 2012.
Hayo yalisemwa jijini
Dar es Salaam jana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara wakati akipokea ripoti ya kamati maalum ya kuratibu
upatikanaji wa vazi la Taifa.
“baada ya kuipokea
ripoti na kuizingatia kwa makini, mapenda sasa kuelekeza hatua za kuchukua ili
mchakato huu wa vazi la Taifa ufikie hatima yake, hata hivyo napenda nichukue
fursa hii kuwapongeza kwa dhati wanakamati ya kwa kazi nzuri mliyoifanya hadi
kufikia hatua hii ya kutoa ripoti”,alisema
Dk.Fenella ameiagiza
Menejimenti ya wizara yake chini ya
usimamizi wa Katibu Mkuu ichague vitambaa vitatu kati ya vitano
vilivyopendekezwa na kamati na hivyo vipelekwe ngazi ya sekretarieti ya Baraza
la Mawaziri, kamati ya ufundi ya makatibu wakuu na hatimaye baraza la Mawaziri.
“Pili waraka wa Baraza
la Mawaziri kuhusu uteuzi wa kitambaa mwafaka
kwa vazi hilo ufikishwe kwenye baraza la mawaziri ifikapo Oktoba 31,
2012...baada ya hapo viwanda vya nguo nchini vihamasishwe kuzalisha kwa wingi
na kwa ubora kitambaa au vitambaa vitakavyokuwa vimeteuliwa ili kushona vazi la
Taifa,”alisema
Awali,Katibu wa kamati
ya vazi la Taifa Angela Ngowi alisema kamati hiyo ilianza kazi yake mwezi
Novemba, 2011 ambapo ilikusanya maoni kutoka kwa wananchi mbalimbali, sambamba
na kutumia vyombo vya habari kuhamasisha kuhusina na zoezi hilo.
Alisema katika mchakato
wa kupata vazi hilo walipokeza zaidi ya michoro 200 kutoka kwa wasanii 88,
kabla ya kamati kupitisha michoro sita ambayo ilikuwa imekidhi vigezo na
kuikabidhi kwa wataalamu wa vitambaa na ndipo wakatoa maamuzi yao.
Kamati ya hiyo ipo
chini ya mwenyekiti wake Joseph Kusaga, huku Angela Ngowi ni Katibu na Wajumbe
ni pamoja na Habibu Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Absalom Kibanda,
Makwaia Kuhenga, na Ndesambuka Merinyo.