KIPA wa timu ya Simba ya Tanzania , Abel Dhaira amepewa unahodha wa timu
ya taifa ya Uganda , Uganda
Cranes kuelekea mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Libya
itakayopigwa kesho.
Uteuzi wa kipa huyo mwenye
umri wa miaka 25, umefanywa na kocha mpya, Milutin 'Micho' Sredojevic, akimweka
kando nahodha wa muda mrefu, Hassan Wasswa.
Wasswa ndie aliiongoza timu
hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Cecafa, mara zote amekuwa akiokewa jukumu hilo na Andy Mwesigwa,
Denis Onyango na Simeone Masaba.
Uteuzi Dhaira, ni wazi
atakuwa kipa wa kikosi cha kwanza badala
ya Onyango anayecheza soka ya
kulipwa katika timu ya Mamelodi
Sundowns.
Wakati Uganda inakabiliwa na mechi dhidi ya Liberia wapinzani wao Libya ,
watakumbana na DR
Congo
kwenye mechi itakayopigwa Juni 8.