Washiriki wa Miss Tabata wakipozi wakiwa safarini kuelekea mbuga za wanyama Mikumi mapema wiki hii.
Na Mwandishi Wetu
Shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013 linafanyika kesho katika ukumbi wa Dar West Park Tabata.
Warembo 20 watachuana kutaka kumrithi Noela Michael ambaye
anashikilia taji hilo
kwa sasa. Noela pia ndiye anashikiria taji la Miss Ilala.
Mbali ya kuwakilisha Miss Tabata kwenye shindano la Miss
Ilala baadaye mwaka huu, mshindi huyo pia atazawadiwa Sh.600,000 pamoja na
king’amuzi kutoka Multichoice ambacho kimelipiwa tayari kwa miezi mitatu kikiwa
na thamani ya Sh.400,000.
Mshindi pili atapata Sh. 300,000, wa nne Sh.200,000 na wa tano atazawadiwa Sh.150,000.
Warembo wengine watakaofanikiwa kuingia 10 bora,
watazawadiwa Sh.100,000 kila mmoja wakati waliosalia watapata kifuta jasho cha
Sh.50,000 kila mmoja.
Warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro hicho mwaka huu ni
Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Upendo Dickson Lema (22),
Hidaya David Mwenda (22), Aneth Ndumbaro (19),
Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa Kitereja (19), Rehema Kihinja (20), Pasilida Mandali (21), Brath Chambia (23),
Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki (20) na Suzan Daniel (18).
Wadhamini wa shindano hilo
ni Dodoma Wine, Redd’s Original, Nipashe, Vayle Springs, Multichoice, Fredito
Entertainment, Integrated Communications Limited, CXC Africa, Brake Point na
Saluti5.
Miss Tabata 2013 imeandaliwa na Bob Entertainment na Keen
Arts.