Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoshirikisha timu
24 zilizogawanywa katika makundi matatu msimu huu (2013/2014) itaanza kutimua
vumbi Septemba 14 mwaka huu.
Kila timu itakayoongoza kundi lake katika ligi itakayochezwa
kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini) ndiyo itakayopanda daraja kucheza Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015.
Mechi za ufunguzi kwa kundi A zitakuwa kati ya Tessema vs
Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam) wakati Septemba 15 mwaka huu
ni Transit Camp vs Polisi Dar (Uwanja wa Mabatini, Pwani), Ndanda vs Friends
Rangers (Uwanja wa Nangwanda, Mtwara) wakati Villa Squad vs African Lyon
itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B ni Burkina Faso vs Polisi Moro (Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro), Mkamba Rangers vs Lipuli (Uwanja wa CCM Mkamba, Morogoro), Majimaji
vs Mlale JKT (Uwanja wa Majimaji, Songea) wakati Septemba 15 mwaka huu Kimondo
SC vs Kurugenzi (Uwanja wa Sokoine, Mbeya).
Mechi za ufunguzi kundi C ni Polisi Mara vs Polisi Dodoma
(Uwanja wa Karume, Musoma), Kanembwa JKT vs Polisi Tabora (Uwanja wa Lake
Tanganyika, Kigoma), Stand United vs Mwadui (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga),
na Pamba vs Toto Africans (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza).
Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Oktoba 26 mwaka
huu wakati wa pili utamalizika Machi 22 mwakani. (Ratiba imeambatanishwa)